Tiba ya siki ya tufaha

Tiba ya siki ya apple

Siki ya Tufaha ni tiba ya harufu ya mwili unaweza kuioga
Watu wengi wamekuwa wakinilalamikia kusumbuliwa na harufu mwilini, hii hapa ni tiba inayotibu tatizo hilo kama una uwezo tumia kwa wiki mara moja au mara mbili kuioga itakusaidia, nasema uwezo kwasababu si rahisi sana kuipata ila ipo na inauzwa maduka makubwa ya vyakula.
Jinsi ya kuoga
Chukua kikombe kimoja au viwili vya siki ya tufaha ‘Apple’ weka kwenye maji ya moto au uvugu uvugu kisha acha kwa muda wa dakika 20 au 30 baada ya hapo chukua nguo iloweke na uusugue mwili wako mwilini, kama sehemu zinazotoa jasho baya unaweza kuosha kwa maji hayo kwanza kisha ndio usugue na kitambaa unachotumia, mfano makwapani, kwenye vidole na pembeni mwa mapaja.
Baada ya hapo acha maji yake yaliyochanganywa na siki yakauke mwili ili kukusaidia kuondoa harufu hiyo.
Siki hii imekuwa ikitumika kutibu vitu vingi, mbali na kukuondolea jasho mwilini pia husaidia kuifanya ngozi yako kung’aa na kuwa na muonekano hai.
***
Vidondoo
Vinegar ya Apple ‘Siki ya Tufaha’ inavyosaidia mambo mengi
Siki ya Tufaha huondoa gesi tumboni
Kama unasumbuliwa na gesi tumboni, tumia kijiko kimoja kidogo cha siki ya tufaha
Jinsi ya kutumia
Chukua maji ya kunywa ambayo si baridi weka kijiko kimoja kidogo kisha kunywa, mbali na aside pia inasaidia kuondoa kiungulia.
***
Siki ya tufaha kwa kutibu mba
Kama unasumbuliwa na mba wa kichwani, ukishaosha nywele zako vizuri zikatakata, chukua maji kidogo changanya na siki ya tufaha kulinganisha na siki yako, kisha paka kuanzia chini kwenye ngozi. Baada ya kupaka acha kwa saa moja au mawili, hii ni tiba ya haraka, kwa kufanya hivi utaona matokeo ndani ya wiki moja au mbili tu.
***
Husaidia kuua fangasi wa ngozi na miguu
Mbali na kutibu mambo yote siki ya Tufaha inasaidia kwenye maambukizi ya fangasi wa mwili hasa hasa wa miguu kwa ujumla.
Jinsi ya kutumia
Chukua kikombe kimoja cha siki changanya na maji yalingane na kikombe hicho kisha paka au nawa kwenye ngozi iliyoathirika, au kwenye miguu katikati, pia inasaidia sana kuondoa tatizo la kubanduka kwa kucha wanaosababishwa na fangasi.
Angalizo: Usithubutu kutumia siki hii bila kuichanganya na maji ni hatari hasa kwa watoto na kwa watu wenye ngozi laini ambayo haihitaji shida za hapa na pale.

Related posts

2 Thoughts to “Tiba ya siki ya tufaha”

  1. Muhamed Salahuddeen

    Nimeipenda post nzuri Sana . Asante kwa kutuelimisha

  2. It’s not my first time to pay a quick visit this web page, i am visiting this website
    dailly and obtain nice facts from here everyday.

    My blog post: Royal CBD

Leave a Comment