About

Tibaasili ni blog iliotengenezwa kwa lengo la kuwawezesha watu kufahamu na kutumia tiba asili kwa wepesi.
Tibaasili inahusisha watu wote wenye uhitaji wa huduma za matibabu haya ambapo watakua wanapata taaluma mbali mbali na pia kununua bidhaa za tibaasili kupitia blog yetu.
Tibaasili kwa upande mwengine inahusisha wataalamu wenye taaluma za tiba asili inayokubalika kisheria ya kiislam isiyo na chembe za shirki, ukiukaji wa sharia za nchi, na udanganyifu. wataalamu watapata fursa ya kuweza kufikia wateja kwa wepesi.
Kazi za blog
Kutoa elimu:
Tiba asili inatoa elimu mbali mbali ya tiba asili ikiwemo magonjwa pamoja na madawa mbali mbali, elimu ambayo imethibitika na inakubalika kisharia,
Wataalamu wetu watakua wanaandaa Makala mbali mbali zinahusu elimu ya afya na matibabu.
Biashara
Tibaasili ina duka la mtandao (ecommerce) ambalo linakuwezesha wewe tabibu kuuza bidhaa zinazohusu tibaa asili kama vile madawa na vitabu, wateja watalipia kisha sisi tutakupatia pesa pamoja na taarifa za mteja kwa ajili ya usafirishaji wa bidhaa kumfikia mteja.
Utambulisho wa matabibu:
Tibaasili inayo kurasa (page) maalumu inayoorodhesha matabibu wetu wote pamoja na taarifa zao, wanapopatikana na mawasiliano yao, ili kuwarahisishia watu wanaohitaji matabibu hao kutokana na matatizo mbali mbali wawapate kwa wepesi.
Faida za kujiunga na tibaasili
• Kuwafikia watu wengi Zaidi:
Blog yetu inasimamiwa na wataalamu wenye weledi wa hali ya juu katika kuiboresha kupatikana kwake, tunataraji kufikia June 2020 blog yetu itakua na watumiaji wasiopungu 100,000 .
Hii itakuongezea nafasi ya watu wengi zaidi na hivyo kuboresha soko la huduma zako.
• Kuaminika:
Moja wa vikwazo vikubwa katika upande wa tibaasili ni kutokuaminika kwa watibabu kutokana na kuwepo kwa wimbi kubwa la matabibu wadanganyifu, blog yetu inahakikisha kila tabibu anaesajiliwa kutoa huduma ni mwaminifu na tiba zake
zinakubalika kisheria, hii itajenga Imani kwa wateja wetu kukuamini kwa vile upo kwenye blog yetu.

Masharti na vigezo

Ili uwe tabibu katika blog yetu ni lazima ukidhi vigezo na masharti yafuatayo:
• Tiba na elimu yako isikinzane na mafundisho ya uislam pamoja na sharia za nchi
• Bidhaa zako ni lazima ziwe zimethibitishwa kutibu na kutokusababisha madhara kwa watumiaji.
• Ili kusajiliwa lazima uwe unatambulika unapofanye kazi na unavielelezo na leseni kutoka mamlaka ya serikali.
• Ni lazima usajiliwe Gutentor Advanced Text