Uzazi wa mpango kwa kutumia kalenda

uzazi wa mpango kwa kutumia kalenda

Kufahamu kuhusu siku za kushika mimba ni muhimu sana kwa wale wanaotaka kupata mtoto na pia wale wanaotaka kudhibiti uzazi,

Kupitia chapisho hili, nitakujuza hatua kwa hatua ni kwa jinsi gani unaweza kutumia njia ya kiasili ya kalenda kufahamu siku ambazo mwanamke anaweza kupata mimba na hivyo kufanya maamuzi sahihi.

Nakusihi usome hadi mwisho na usiache kuuliza kwa ku comment kama kuna lolote unataka kufahamu zaidi, pia share kwa wengine na wao wapate faida.

Kuhusu uzazi wa mpango kwa kutumia kalenda:

Ili kuitumia njia hii kwa mafanikio makubwa unahitaji kujua siku zako za kushika mimba katika mwezi (Fertile Window):

Siku za kushika mimba ni sita (6) katika kipindi cha mzunguko wa mwezi.

  • Siku tano  (5) Kabla ya yai la mwanamke kutoka (Ovulation)
  • Siku moja (1) kuanzia yai linapotoka (masaa 24)

Baada ya siku hizi hakuna uwezekano wa mwanamke kushika mimba.

Ni siku gani mbegu ya mwanamke inatoka (Ovulation)?

Utafiti inaonyesha ya kwamba siku ya kumi na nne kuanzia siku ya mwanzo ya hedhi kurudi nyuma ndio siku ya kutoka yai.

Ina maanisha baada ya yai kutoka huchukua siku kumi na nne hadi kutoka kwa hedhi.

Hivyo basi, kwa mfano mwanamke alipata hedhi tarehe ishirini (20) ukitoa siku kumi na nne nyuma  utapata yai lilitoka tarehe 6.

Kwa maana hiyo mwanamke huyu siku zake za kushika mimba (fertility window) ni kuanzia tarehe moja (siku tano kabla) pamoja na masaa ishirini na nne ya siku ya kutoa yai (terehe 6).

Kabla ya tarehe moja na baada ya tarehe sita hakuna uwezekano wa kupata mimba.

Ufafanuzi juu ya siku za kushika mimba.

  • Siku ya tano kabla ya siku ya kuteremsha yai (ovulation)

Inakisiwa ya kwamba mebu za kiume (sperm) wanauwezo wa kuhimili kuishi kati ya siku nne hadi tano.

Baada ya kujamiiana sperm husafiri hadi katika sehemu ya kutunga mimba ya mwanamke (fallopian tube), endapo yai la uzazi la mwanamke litakuwepo hapo mbegu mbili hizo huungana(fertilization) na kutunga mimba.

Iwapo mbegu ya kike (Ovum) haikuwepo, mbegu za kiume zitabaki kusubiri kati ya siku nne hadi tano baada ya siku tano mbegu hizo zitakufa na hakutakua na uwezekano wa kutunga mimba.

Hii inatufahamisha ya kwamba,  ili kudhibiti mimba mwanamke kwanza anahitaji kufahamu siku yake ya kutoa mbegu ili ajizuie au kutumia njia mbadala siku tano kabla yake.

  • Siku moja (1) kuanzia yai linapotoka (masaa 24)

Mbegu ya uzazi ya mwanamke (Ovum) inapotoka kutokea kwenye Ovary husafiri hadi kufikia sehemu ya kutunga mimba(fallopian tube) hapo hukaa kusubiri mbegu za kiume ili kutunga mimba, huchukua masaa ishirini na nne tu baada ya hapo huteremka na hakuna uwezekano tena wa kutunga mimba.

Kufahamu siku ya kuteremsha mbegu ya kike kupitia mizunguko tofauti tofauti.

Wanawake wanatofautiana katika mzunguko wa hedhi.

Kwa idadi yoyote hile ya siku za mzunguko ulio nao la kuzingatia kipindi cha mbegu ya mwanamke ni siku kumi na nne kwa watu wote hivyo cha muhimu ni kufanya uchunguzi wa mzunguko wako alau kwa muda wa miezi mitano au sita kupata kujua ni tarehe gani unaingia katika hedhi.

Baada ya kupata tarehe yako hesabu siku kumi na nne kurudi nyuma kujua siku ya yai kutoka yai ukifahamu siku yako ya kutoa yai utaweza kudhibiti uzazi kupitia utaratibu uliotangulia hapo juu.

Tanbihi.

Njia hii uzazi wa mpango kwa kutumia kalenda ili iweze kufanya kazi na kuleta matoke mazuri

Kwa wale ambao mizunguko yao inabadilika mara kwa mara haieleweka, njia hii kwao si muafaka hivyo wajaribu kutumia njia nyengine  mbadala za asili zisizo na madhara kama vile kumwaga nje hadi mizungoko yao ikae sawa.

Pia hakikisha umefanya utafiti wa kutosha alau miezi mitano kuhusu mizunguko yako ya miezi.

Related posts

Leave a Comment