Tiba ya Kwikwi
Habari ndugu yangu. Karibu Tiba asili, Kupitia post hii leo utajifunza tiba ya Kwikwi,Kwikwi ni kitu gani?
Kwikwi (Kekefu) ni hali ya kushtuka na kusinyaa kwa ghafla kwa misuli mikuu ya upumuaji (diaphragm) ambako hujirudia rudia na kusababisha hewa kuingia kwa kasi kwenye mapafu. Hali Hii husababisha milango ya sauti katika koo (vocal cords or voice making cords) kufunga ghafla na kutoa sauti inayosikika wakati wa kwikwi. Kwikwi sio ugonjwa, kwikwi ni ya muda mfupi ambayo inapita, lakini kwikwi isiyokatika inaweza kuwa dalili ya tatizo lingine ambalo huenda likahitaji uchunguzi wa kitaalamu.Sababu zinazopelekea tatizo la kwikwi
-
- Kula haraka haraka au kula sana (kuvimbiwa)
-
- Kula vyakula vyenye viungo sana (very spicy foods)
-
- Kunywa vinywaji vyenye gesi(carbonated beverages) au vya baridi sana
-
- Ulevi au kunywa pombe nyingi kwa mpigo
-
- Upungufu wa maji na madini mwilini (dehydration)
-
- Tumbo kujaa gesi, asidi (hyperacidity) au vidonda vya tumbo
Tiba ya kwikwi kwa kutumia kitunguu maji (anion):
Kitunguu maji(anion) ni Mujarrab sana kwa magonjwa mengi likiweo tatizo la kwikwi. Tiba ya kwikwi kupitia kitunguu maji ni kama ifuatavyo:- Kata kata kisha ponda kitunguu maji kutumia kinu, blender, au chochote kile hadi kipondeke vizuri.
- Weka chumvi na maji machache kisha changanya vizuri
- Kamua na kisha chuja mchanganyiko wako upate juisi.
- Weka kwenye Chombo safi kisha kunywa utapata matokeo mazuri hapo hapo kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu.