Kitunguu Maji Tiba ya Kwikwi (Hiccups)

Dawa Ya Kwikwi (Hiccups)

Karibu upate taaluma. Tafdhali soma Hadi mwisho kuna maelekeo ya jinsi Kituunguu maji kinavyotibu tatio la Kwikwi :

Kwikwi (Kekefu) hutokea kutokana na kushtuka na kusinyaa kwa ghafla kwa misuli mikuu ya upumuaji (diaphragm) ambako hujirudia rudia na kusababisha hewa kuingia kwa kasi kwenye mapafu.

Hii husababisha milango ya sauti katika koo (vocal cords or voice making cords) kufunga ghafla na kutoa sauti inayosikika wakati wa kwikwi.

Kwikwi sio ugonjwa; kwikwi ya muda mfupi ni kero ndogo tu ambayo inapita, lakini kwikwi isiyokatika inaweza kuwa dalili ya tatizo lingine ambalo huenda likahitaji uchunguzi wa kitaalamu.

Baadhi Ya sababu zinazopelekea tatizo la kwikwi

  • Kula haraka haraka au kula sana (kuvimbiwa)
  • Kula vyakula vyenye viungo sana (very spicy foods)
  • Kunywa vinywaji vyenye gesi(carbonated beverages) au vya baridi sana
  • Ulevi au kunywa pombe nyingi kwa mpigo
  • Upungufu wa maji na madini mwilini (dehydration)
  • Tumbo kujaa gesi, asidi (hyperacidity) au vidonda vya tumbo

Namna ya kutibu kwikwi kwa kutumia kitunguu Maji:

  • Ponda kitunguu maji hadi kichachagike
  • Weka chumvi na maji machache
  • Kamua na chuja upate juisi kupitia mchanganyiko huo
  • Weka kwenye Chombo safi kisha kunywa Utapata matokeo mazuri hapo hapo kwa uwezo wa Mungu.

Tafadhali Share Makala hii. ahsante

Related posts

Leave a Comment